Tuesday, 16 December 2008
HABARI NDIO HIYO
Jamani habari ndio hiyo....will keep you updated.
Kumbuka UKIMWI BADO UPO.
Monday, 8 December 2008
JE, DAWA ZA UKIMWI ZA KUONGEZA MIAKA YA KUISHI, ZINACHANGIA KATIKA KUAMBUKIZWA KWA WATU ZAIDI?
Mimi naona madawa yanatengenezwa kwa madhumuni ya kuponyesha na kukinga magonjwa kwa wale walioambukizwa na kwa wasioambukizwa. Watu hawa ambao wanatumia madawa haya hupewa miaka zaidi ya kuishi, na haihusiani kabisa na kuongezeka kwa ugonjwa huu. Wale wanaoambukiza wengine kwa makusudi wanatakiwa kuchukuliwa sheria. Sijui wanajamii mnaonaje kuhusu suala hili.
Tuesday, 2 December 2008
KUTENGWA NA HOFU JUU YA WATU WENYE UKIMWI, INASAIDIA KUONGEZEKA KWA MAAMBUKIZO
- Kwanza, watu wenye maambukizo haya ya ukimwi hulaumiwa kwa kupata ugonjwa huo, na watu wengi huamini kwamba yule aliyeambukizwa angeweza kuepukana na ugonjwa huo kama angefanya maamuzi mazuri.
- Pili, ingawa ugonjwa huu una madawa ya kusaidia virusi hivyo visisambae mwilini kwa haraka, lakini hakuna matibabu ya kuviua kabisa.
- Tatu, kuna ufinyu wa kotojua njia ya usambazwaji wa virusi vya ukimwi mwilini, na hii inawafanya watu wengi watishwe zaidi na gonjwa hili.
Hofu juu ya watu wenye ukimwi inasababishwa na watu ambao wanaiacha ikue ndani ya mioyo yao kutokana na uoga wao wenyewe. Hofu juu ya ukimwi/virusi inajibainisha yenyewe kwa njia tofauti kama, kumfukuza mtu kazi, nyumbani, au hata kuonewa kwa sababu umegundua ana ukimwi.
China na UNAIDS, wamekemea suala la hofu na kutengwa kwa watu wenye ukimwi. Kwamba kama watu walioathirika na ukimwi wasingetengwa na kudhalilishwa, na ugonjwa huu uonekana ni kama ugonjwa wa cancer au magonjwa mengine, hii ingesaidia kuwafanya watu wengi zaidi kwenda kupima na kuanza matibabu mapema. Kutengwa na kutothaminiwa kwa watu walioathirika inawezekana ndio inawapa hasira waathirika hawa na kuwafanya walipize kisasi kwa kuchukua maamuzi ya kuusambaza ugonjwa huu.
Je mdau unaonaje hili swala, je ni kweli watu wanasambaza ukimwi kutokana na kutengwa na kutothaminiwa na jamii.
Naomba maoni yenu.
Monday, 1 December 2008
JE UNAJUA UNAWEZA KUTOMUAMBUKIZA MTOTO UKIMWI AKIWA TUMBONI
Maambukizo haya kwa mtoto yanaweza kutokea katika kipindi cha mimba, uchungu, kuzaa ama wakati wa kunyonyesha. Bila matibabu kadilia ya asilimia 30% ya watoto huzaliwa na maambukizo katika kipindi cha mimba au kuzaa, na karibu asilimia 20 ya watoto huambukizwa kwa njia ya kunyonyesha.
Tafadhali bonyeza kwenye hii link ina maelezo mengi mazuri yanaweza kusaidia: http://www.avert.org/motherchild.htm.
SIKU YA UKIMWI DUNIANI, JE UKO SALAMA?
UNAIDS inakadilia kwamba mpaka sasa kuna watu milioni 33.2 duniani wanaoishi na virusi vya ukimwi, kati ya hao milioni 2.5 ni watoto. Pia wanakadilia watu milioni 2.5 wameathirika kwa kipindi cha mwaka 2007 tuu. Nusu ya watu wanaoishi na ukimwi duniani ni vijana waliopata maambukizo hayo wakiwa chini ya miaka 25, na hufa kabla ya kufikia miaka 35. Karibu asilimia 95 ya watu wenye ugonjwa wa ukimwi/virusi vya ukimwi wanaishi kwenye mataifa ya kimasikini duniani, lakini virusi vya ukimwi leo ni tishio kwa watu wa jinsia zote na watoto duniani kote.
Siku ya ukimwi duniani ilianza tarehe 01/12/1988, naomba watanzania wenzangu tuelimike kuhusu ukimwi na tujue kwamba ukimwi bado upo na unaweza kunipata mimi, wewe na yule. Watanzania safari bado ni ndefu.