Monday, 8 December 2008

JE, DAWA ZA UKIMWI ZA KUONGEZA MIAKA YA KUISHI, ZINACHANGIA KATIKA KUAMBUKIZWA KWA WATU ZAIDI?

Sijui wewe unaonaje kuhusu hili swala. Juzi nilikutana na mtu ambaye katika mazungumzo juu ya ukimwi na maambukizo aliniuliza swali hili; "Dada hauoni kwamba madawa ya ukimwi yanasaidia kuongezeka maambukizo"? Akimaanisha kwamba watu wanaotumia madawa haya huongezewa miaka ya kuishi na kwa kufanya hivyo inaongeza namba ya wanaoambukizwa kila siku endapo watu hawa wataendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wengine wasioathirika. Sana sana Afirika, hakuna sheria yeyote ile inayomsitisha mtu mwenye ukimwi kumuambukiza kwa makusudi mwingine asiyeathirika.

Mimi naona madawa yanatengenezwa kwa madhumuni ya kuponyesha na kukinga magonjwa kwa wale walioambukizwa na kwa wasioambukizwa. Watu hawa ambao wanatumia madawa haya hupewa miaka zaidi ya kuishi, na haihusiani kabisa na kuongezeka kwa ugonjwa huu. Wale wanaoambukiza wengine kwa makusudi wanatakiwa kuchukuliwa sheria. Sijui wanajamii mnaonaje kuhusu suala hili.

No comments: