Monday 1 December 2008

SIKU YA UKIMWI DUNIANI, JE UKO SALAMA?

leo ningependelea kuwakumbusha watanzania umuhimu wa kutumia CONDOMS ili kujiepusha na magonjwa ya zinaa haswa UKIMWI. Hii ni kwa sababu leo ni siku ya ukimwi duniani na ningependa wote tuungane na watu wote duniani kuwakumbuka ndugu jamaa na marafiki waliokufa kutokana na gonjwa hili ambalo bado halijatafutiwa ufumbuzi. Kumbukumbu hii ituelimishe na kutupa tahadhari juu ya ukimwi.

UNAIDS inakadilia kwamba mpaka sasa kuna watu milioni 33.2 duniani wanaoishi na virusi vya ukimwi, kati ya hao milioni 2.5 ni watoto. Pia wanakadilia watu milioni 2.5 wameathirika kwa kipindi cha mwaka 2007 tuu. Nusu ya watu wanaoishi na ukimwi duniani ni vijana waliopata maambukizo hayo wakiwa chini ya miaka 25, na hufa kabla ya kufikia miaka 35. Karibu asilimia 95 ya watu wenye ugonjwa wa ukimwi/virusi vya ukimwi wanaishi kwenye mataifa ya kimasikini duniani, lakini virusi vya ukimwi leo ni tishio kwa watu wa jinsia zote na watoto duniani kote.

Siku ya ukimwi duniani ilianza tarehe 01/12/1988, naomba watanzania wenzangu tuelimike kuhusu ukimwi na tujue kwamba ukimwi bado upo na unaweza kunipata mimi, wewe na yule. Watanzania safari bado ni ndefu.

No comments: