Tuesday, 2 December 2008

KUTENGWA NA HOFU JUU YA WATU WENYE UKIMWI, INASAIDIA KUONGEZEKA KWA MAAMBUKIZO

Ndugu mtanzania, sijui wewe unaonaje kuhusu hili swala la kuwatenga, kuwatusi, kuwashusha, na kutothaminika kwa watu wenye virusi vya ukimwi. Hii kwa lugha ya kabila jingine wanaita "HIV/AIDS Stigmatism" . Hii inatokana na tabia, mazoea, imani, sera za watu juu ya wale walioambukizwa na ukimwi, pia juu ya ndugu, marafiki, jumuia au watu wa karibu wa mtu aliyeambukizwa na ukimwi. Hii inatokana na vitu vifuatavyo:

  • Kwanza, watu wenye maambukizo haya ya ukimwi hulaumiwa kwa kupata ugonjwa huo, na watu wengi huamini kwamba yule aliyeambukizwa angeweza kuepukana na ugonjwa huo kama angefanya maamuzi mazuri.
  • Pili, ingawa ugonjwa huu una madawa ya kusaidia virusi hivyo visisambae mwilini kwa haraka, lakini hakuna matibabu ya kuviua kabisa.
  • Tatu, kuna ufinyu wa kotojua njia ya usambazwaji wa virusi vya ukimwi mwilini, na hii inawafanya watu wengi watishwe zaidi na gonjwa hili.

Hofu juu ya watu wenye ukimwi inasababishwa na watu ambao wanaiacha ikue ndani ya mioyo yao kutokana na uoga wao wenyewe. Hofu juu ya ukimwi/virusi inajibainisha yenyewe kwa njia tofauti kama, kumfukuza mtu kazi, nyumbani, au hata kuonewa kwa sababu umegundua ana ukimwi.

China na UNAIDS, wamekemea suala la hofu na kutengwa kwa watu wenye ukimwi. Kwamba kama watu walioathirika na ukimwi wasingetengwa na kudhalilishwa, na ugonjwa huu uonekana ni kama ugonjwa wa cancer au magonjwa mengine, hii ingesaidia kuwafanya watu wengi zaidi kwenda kupima na kuanza matibabu mapema. Kutengwa na kutothaminiwa kwa watu walioathirika inawezekana ndio inawapa hasira waathirika hawa na kuwafanya walipize kisasi kwa kuchukua maamuzi ya kuusambaza ugonjwa huu.

Je mdau unaonaje hili swala, je ni kweli watu wanasambaza ukimwi kutokana na kutengwa na kutothaminiwa na jamii.

Naomba maoni yenu.

No comments: