Tuesday, 16 December 2008

HABARI NDIO HIYO

Jamani leo nimesoma news moja inayotoa matumaini kwenye utafiti wa dawa ya ukimwi. Wanasayansi huko Pennsylvania Marekani wameweza kupunguza idadi ya virusi ndani ya nyani vinavyofanana na vya ukimwi vijulikanavyo kama simian immunodeficiency virus(SIV). SIV ni virusi vya ukimwi lakini vinazuru wanyama tuu na sio binadamu. Wanasayansi hao wameweza pia kuongeza maisha ya nyani huyo aliyekuwa ameathirika na ukimwi. Wanasayansi hayo wamefanikiwa kufanya hivyo baada ya kuziba receptor molecule ijulikanayo kama Programme Death-1 (PD-1) ambayo huzuia kazi kwa immune system yetu ipiganayo na virusi vya ukimwi. Kwa kuziba hiyo PD-1, kunachochea cells za ulinzi wa mwili (CD8 T cells) zipigane na wadudu wa ukimwi na hivyo hupunguza idadi ya kuzaliana kwa wadudu hawa. Kwa habari zaidi bonyeza hapa

Jamani habari ndio hiyo....will keep you updated.

Kumbuka UKIMWI BADO UPO.

1 comment:

Anonymous said...

Sasa mrembo mbona ujaweka Contact zako?tunamengi ya kuelezea juu ya maisha na Ukimwi ili kuwaelemisha vijana wenzetu.weka contact zako ili tuweze kukupa ushauri juu ya nini utuandalie kwenye website yako.
Asante
Flavie De Karate